Counties

Wananchi Migori waombwa kukomesha dhuluma za kijinsia

Spread the Word
GBV
GBV

Wananchi kaunti ya Migori wameombwa kuwa mstari wa mbele kukomesha visa vya dhuluma za kijinsia.

Hii ni kwa kuwakamata na kuwasalimisha kwa vyombo vya usalama kama njia moja wapo ya kupigania haki za kijinsia.

Akizungumza mjini Kehancha katika hafla ya kuhamasisha wananchi dhidi ya kuendeleza dhuluma za kijinsia Naibu Kaunti Kamishna wa Kuria Magharibi Andrew Mwiti alisema kuwa wananchi wanauhuru wa kumshika na kumwasilisha kwa vyombo vya dola yeyote atakaye patikana hasaa akimdhulumu mama na mtoto wa kike.

Vile vile aliwaraia wakaazi hasaa eneo la kuria kutibua mipango yeyote ya kukeketa mtoto wa kike pasi na kungoja maafisa wa usalama.

Kwa upande wake Wakili Esther Ang’awa aliwarai wananchi kutoogopa kutoa ripoti za dhuluma za kijinsia kwani serikali inashirika la kuwalinda mashahidi wote almaarufu Witness Protection Agency.

Wakili huyo alisema kuwa mara nyingi, wananchi huogopa kutoa ripoti za visa hivi kwa kuogopa kuandamwa na washukiwa.

DO YOU HAVE MORE?

Send TIPS/Opinion to  news@payuka.co.ke You can also find us on Facebook

Leave a Reply